KUHUSU WAJIBU

NMB inaamini kwamba watoto na vijana ni taifa la kesho, na ni muhimu kuwajengea mazingira mazuri ya kifedha ili kuwawezesha kufikia ndoto zao. Hii ndiyo sababu ya kushirikiana na Women’s World Banking kuzindua WAJIBU – akaunti za akiba kwa ajili ya watoto na vijana zinazowajenga kwenye elimu ya kifedha na kifikra kuelekea katika mafanikio yao ya baadae.

BARABARA YA ELIMU YA KIFEDHA – AKAUNTI TATU ZA AKIBA MUHIMU KWA MTOTO WAKO.

Mtoto Akaunti

Tunakusaidia kuweka akiba ya mwanao aliye na miaka 0 -17 kwa baadae.

Chipukizi Akaunti

Tunamsaidia kijana kupanga malengo yake akiwa na akaunti inayomfaa.

Mwanachuo Akaunti

Tunakupa urahisi wewe mwanachuo kuweka akiba ya baadae.

 

 

 

 

TUNAMTAMBULISHA JOHARI

Johari ni binti mdogo wa miaka 9 anayetambua umuhimu wa kuweka akiba na mwenye ndoto za kufanikiwa. Anaelewa manufaa ya kuweka akiba kwa ajili ya kufikia lengo fulani na ndiyo maana kiasi kikubwa cha pesa za matumizi anazopatiwa na wazazi wake anahifadhi kwenye akiba yake binafsi. Akiba yake imemsaidia kununua begi jipya la shule. Amefurahi zaidi kufunguliwa akaunti ya Mtoto ya Wajibu. Ana ndoto za kuwa na mafanikio makubwa baadae.

 

JIUNGE NA HARAKATI

Jiunge na harakati zetu za Wajibu kama hatua kubwa kuelekea kwenye mafanikio makubwa ya uratibu wa fedha. Ukiwa nasi utapata dondoo za kila wiki na kila mwezi kuhusu promosheni na ofa zetu pamoja na ushauri wa uratibu wa pesa.

Taarifa na anuani zako zitakuwa salama na hazitatumika vibaya.